Latest Post



Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Abel Makubi akikagua wodi ya wanaume iliyoko hospitali ya rufaa ya mkoa Dodoma.Kushoto ni Muuguzi Mfawidhi wa hospitali hiyo Stanley Mahumbo.

Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Abel Makubi akikagua duka la dawa la Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma.
Mganga Mkuu wa Serikali akitazama moja ya faili la   mgonjwa aliolazwa kwenye wodi hiyo ambapo alibaini mapungufu.

Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Abel Makubi akiangalia moja ya mashine zilizopo kwenye maabara ya hospitali hiyo.

Na. WAMJW-Dodoma

Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Abel Makubi ameuagiza Uongozi wa  Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma kuboresha huduma za tiba kwa wananchi wanaofika kupata huduma za afya katika hospitali hiyo.

Prof. Makubi ametoa maagizo hayo kufuatia ziara ya kushtukiza aliyoifanya kwenye Hospitali hiyo na kushuhudia changamoto mbalimbali ikiwemo baadhi ya wagonjwa kuchelewa kupewa huduma, Madaktari bingwa kutowaona wagonjwa kwa wakati na huduma za vipimo kuchelewa.

“Yapo mazuri tumeona mnayofanya kwa wananchi na tunawapongeza, ila lazima kuangalia upande wa pili ambao wananchi wanayataka, kwa yale mapungufu tuliyoyaona tungependa kuona yanaboreshwa haraka ili hospitali hii iwe ya mfano kwa hospitali zote za rufaa za mikoa kwa kutoa huduma zilizo bora”.

Prof. Makubi amesema hospitali hiyo inatakiwa kuonesha mfano kuanzia utoaji wa huduma bora kwa mteja pamoja, kupunguza muda wa wagonjwa kusubiri huduma, upatikanaji wa wauguzi na mabingwa wanapohitajika na usafi wa wodi kwani ndiyo chachu ya wananchi wengi kufika hapo na kupata huduma kabla hawajapewa rufaa ya kwenda Hospitali kubwa kama Benjamin Mkapa.

Aidha, Mganga Mkuu huyo ameutaka uongozi na watumishi wa hospitali hiyo kutambua majukumu yao  kwa kuonesha kuwajali wananchi  wote na kuwataka kuweka utaratibu usio na usumbufu kwa wagonjwa na kupatiwa huduma kwa wakati.

Prof. Makubi alionyesha kusikitishwa alipokuta wodini  baadhi ya wagonjwa wamelazwa na hawajaonwa na Mabingwa kwa zaidi ya siku tatu, wauguzi wakiwa hawajaambatana na madaktari katika kuzungukia wagonjwa huku madaktari wa vitendo (interns)  wakifanya “procedures” peke yao bila uangalizi na baadhi ya  wagonjwa wengine wakiwa wamelazwa chini wakati vitanda viko wazi pamoja na mazingira ya wodi hayakuwa ya kuridhisha na kukosekana kwa mpangilio wa vifaa (5S)

 “Lazima watumishi mjitambue mko wapi kwani awamu hii ni ya kuwajali wanyonge na kufanya kazi  kwa bidii ndio kanuni ya awamu hii hapa kazi tu”. Alisisitiza Prof. Makubi.

Prof. Makubi ameelekeza madaktari wa hospitali hiyo kufanya kazi kwa ushirikiano na wauguzi katika kuwahudumia wagonjwa katika wodi, kuleta mabadiliko kwa kutengeneza miongozo mbalimbali ya kusimamia huduma na kuacha kufanya kazi kwa mazoea ili kila mwananchi anayefika hospitalini hapo ahudumiwe kwa wakati na huduma inayostahili.

Kwa upande mwingine Mganga Mkuu huyo wa Serikali ameitaka hospitali hiyo kuboresha idara ya huduma kwa wateja (Customer Care) kwani hakuna mgonjwa anayependa kuchelewa kupata huduma hivyo lazima kutoa huduma bora na zinazohitajika kwa wananchi wote.

Prof. Makubi ameelekeza Uongozi wa Hospitali kuhakikisha mashine za maabara ambazo zimeishiwa vitendanishi, zinaanza kufanya kazi haraka.

"Ni vizuri mkapunguza muda wa kusubiri majibu ya vipimo vya damu, X-ray, ultrasound, na Moyo na vipimo vingine".Alielekeza Prof. Abel Makubi.

Prof. Makubi aliagiza Hospitali zote nchini zifanyie kazi changamoto alizoziona hapo Dodoma, na akaagiza Idara ya ukaguzi wa huduma bora kutoka wizarani wafanye ufuatiliaji wa utoaji wa huduma mikoani,  wilayani na Vituo vya afya kila mwezi na kutoa taarifa kwake.


Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Abel Makubi akiongea na wataalam kutoka Wizara ya Afya na TAMISEMI wakati wa kujadili utoaji wa huduma bora za afya kwenye vituo vya afya,hospitali za halmashauri na rufaa zilizojengwa kukarabatiwa na Serikali
Mkurugenzi wa huduma za Afya, Lishe na Ustawi wa Jamii-TAMISEMI Dkt. Ntuli Kapologwe akiongea wakati wa kikao hicho.
Mkurugenzi wa Idara ya Kinga kutoka Wizara ya Afya Dkt. Leonard Subi akiwasilisha mada wakati wa kikao baina ya Wizara ya Afya na TAMISEMI






Na. WAMJW-Dodoma

Serikali imefanikiwa kutimiza dhamira ya kuhakikisha kunakuwa na upatikanaji na uwiano wa kutosha katika utoaji huduma za afya pamoja na kuhakikisha wananchi wanapata huduma za afya za uhakika na wakati.

Hayo yamesemwa leo na Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Abel Makubi wakati akifungua kikao kati ya Wizara ya Afya na Ofisi ya Rais-TAMISEMI cha kujadili utoaji huduma bora za afya kwenye vituo vya afya, Hospitali za Halmashauri na Rufaa zilizojengwa na kukarabatiwa na serikali ya awamu ya tano.

“Sisi kama wataalam tunawajibu wa kuendeleza chachu ya maendeleo  yaliyofikiwa na kuhakikisha vituo hivi vinafunguliwa kwa kuzingatia utaratibu unaotakiwa na kuendelea kutoa huduma vikiwa na vifaa vyote muhimu na wataalam wenye weledi na stadi katika kupambana na magonjwa na kupunguza vifo vinavyozuilika”.Amesema Prof. Makubi.

Prof. Makubi ameongeza kuwa mafanikio hayo yamepatikana kufuatia sekta ya afya kuchukua jukumu la kufanya ukarabati wa ujenzi katika vituo vya kutolea huduma za afya ambapo iliweka kipaumbele kwenye vituo vya afya vya msingi ili kuviwezesha kutoa huduma za dharura za uzazi na mtoto mchanga.

“Tumejenga hospitali mpya za wilaya 99, kutoka hospitali 70 za awamu ya kwanza zimekamilika na nyingi zimeanza kutoa huduma hata hivyo serikali imeongeza kujenga hospitali nyingine 29 na fedha zake zimetengwa tayari”. Ameongeza Prof. Makubi.

Awali akiongea kwa niaba ya Naibu katibu Mkuu wa Afya TAMISEMI, Mkurugenzi wa huduma za Afya, Lishe na ustawi wa jamii Dkt. Ntuli Kapologwe amesema kuwa kikao hicho kina lengo la kuwa na muelekeo mzuri wa sekta ya afya hivyo ushirikiano wa pamoja kati ya Wizara hizo mbili ni muhimu katika kufanikisha na kusukuma mbele sekta hiyo nchini.

Naye Mkurugenzi wa huduma za kinga kutoka Wizara ya Afya Dkt. Leonard Subi amesema kuwa vituo vya afya 570 vilivyojengwa na kukarabatiwa na Serikali vimeweza kuboresha huduma za afya na kuzuia vifo vya akina mama wajawazito na watoto wachanga huku vikiwa na uwezo wa kutoa huduma za dharura kama upasuaji.

MWISHO

Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu akiongozana na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Bw. Gelasius Byakanwa wakikagua ujenzi wa Hospitali mpya ya kanda ya kusini inayojengwa Mkoani Mtwara.

Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu akisikiliza maelezo kutoka kwa msanifu majengo anayesimamia mradi wa ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya kanda ya kusini wakati alipotembelea Hospitali hiyo kuona hali ya ujenzi.

Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu akiwa na Mbunge wa Mtwara vijijini Mhe. Hawa Ghasia wakitembelea ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya kanda ya kusini iliyopo Mtwara.


Sehemu ya jengo la Hospitali ya Rufaa ya Mikoa ya kusini inayoendelea na ujenzi.

Na. WAJMW-Mtwara

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu ametembelea ujenzi wa Hospitali mpya ya Rufaa ya Mikoa ya kusini iliyopo mkoani Mtwara na kuridhishwa na kasi ya ujenzi wa Hospitali hiyo.

Waziri Ummy ameonekana kuridhidhishwa na ujenzi wa Hospitali hiyo ambao umefikia asilimia 80 na inagharimu Shilingi Bilioni 15.8 mpaka kukamilika kwake.

"Kukamilika kwa Hospitali hii kutasaidia kupunguza rufaa kwa wananchi wa mikoa ya kusini kwenda kutafuta huduma za kibingwa Muhimbili, MOI au JKCI, huduma zote zitakua zinapatikana hapa". Amesema Waziri Ummy.

Waziri Ummy amesema lengo la Wizara ya Afya ni kuona huduma zinaanza kutolewa katika Hospitali hiyo kabla ya kuanza kampeni za uchaguzi mwaka huu kwani ilikua ni ahadi ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli alipopita mwaka 2015 kuomba kura na Hospitali hiyo ipo kwenye utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi.

"Hatutaki watu wa Mtwara na mikoa ya kusini kwa ujumla muende Dar Es Salaam kwa ajili ya kufuata huduma za CT-Scan, huduma za madaktari bingwa ikiwemo upasuaji wa mifupa, mishipa ya fahamu, Madaktari wa watoto na uzazi. Huduma zote hizi zitapatikana hapa mara baada ya ujenzi wa Hospitali hii kukamilika". Amesema Waziri Ummy.

Waziri Ummy amesema kwa ujumla hali ya sekta ya Afya mkoani Mtwara ni nzuri ambapo katika kipindi cha miaka mitano Hospitali mpya za Wilaya tatu zimejengwa ambazo ni Nanguluwe, Nanyamba pamoja na Masasi. Aidha, vituo vya Afya vinane vimejengwa katika Mkoa huo katika kipindi hicho na kufanya idadi kufikia vituo 23 kutoka 15 wakati Rais Magufuli anaingia madarakani.




Je unajua kuwa tabia ulizonazo ni kutokana na kundi lako la damu?

Kwa kawaida kila binadamu yuko kwenye kundi mojawapo la damu kati ya makundi manne A,B,AB na O.

Makundi haya yanaweza kutumika kufahamu tabia za binadamu na jinsi hii yaweza kuwa rahisi na ya karibu zaidi kuliko kutumia nyota “astrology” kama ambavyo wengi wanafanya, na wataalamu wanasema tabia kwa 

uhusiano na kundi la damu ina uhakika zaidi kuliko wenye vyanzo vingine. Mbali na tabia, ukweli ni kwamba makundi yetu ya damu yanaweza kutuonyesha pia vile mtu anavyopendelea na asivyopendelea,

kazi anazopendelea, watu anaowapendelea na hata vyakula. Baadhi ya watafiti nchini korea wamebainisha kuwa hata namna tunavyopendelea kuketi hutegemea sana na makundi yetu ya damu, sasa tuangalie uhusiano huu

Damu kundi “A”

Hawa watu maranyingi huwa mifano ya kuigwa na wengi kwasababu ya kiu zao na upiganaji wao kwenye mafanikio, ni watu wema,wapole na wenye tabia njema. 

Pamoja na hayo ni rahisi sana watu hawa kupata msongo wa mawazo “stress” na kufikiria sana vitu. Wakiamua kujitoa kwa ajili ya kumsaidia mtu basi wanazama kabisa na wanaweza hata kujisahau wao.

Mazuri yao

Ni watu wanaopenda vitu vikamilike katika hali ya juu “perfectionists”, wanapenda mpangilio maalumu, wanapenda na wanaweza kuchambua mambo sawia, wanawajibika na kubeba majukumu yao,wana huruma na wako tayari kusaidia, waaminifu, ni wagunduzi, wanamaanisha, wavumilivu, na wenye tabia njema.

Mapungufu yao

Wasumbufu,wana hisia kali hata kwenye vitu vya kawaida, wakitaka kitu wametaka, wengine wana aibu,wengine wakimya zaidi na wanaopenda kujichanganya.
Kwenye maisha ya kijamii
Ni mtu ambaye unaweza kumwamini na kumtegemea
Anajali na kumaanisha

Wakati wote huepuka shari,misuguano na magomvi
Maranyingi hawapendezwi wala kufurahia sherehe zenye makelele na shangwe za ajabu ajabu,wanapendelea ukimya na utulivu.
Kazini

Unaweza kumwamini na kumtegemea katika majukumu
Wanapenda ufanisi wa kiwango cha juu kwahiyo kazi zao mara nyingi ni bora sana.

Bahati mbaya wanajali sana hata vitu vilivyo vidogo nahii huwafanya kuwa na msongo wa mawazo kirahisi.
Wasio waelewa vema watu wa kundi hili wanaweza kupata shida kufanya nao kazi
Kwenye mahusiano na mapenzi
Ni ngumu kidogo wao kufunguka na kushirikisha mambo yao.

Wanaweza kuonekana wenye aibu, au waoga.
Ukitaka kumchumbia au kuchumbiwa na mtu wa kundi ‘A’ unahitaji uvumilivu.

Wakiamua kupenda utawafahamu wakati wote na ingawa watakuruhusu ufahamu tu yale maeneoa ya maishani mwao ambayo wanajua unahusika, hawawi wazi katika kila eneo.

Ukweli mwingine kuhusu watu wa kundi ‘A’
Ni watu wabunifu na wenye ujuzi wa usanii “artists”
Wanalewa kirahisi sana, kilevi kidogo tu kitampelekesha sana
Wengi wao hupendelea kula mboga mboga “vegetarians”

Damu kundi “B”

Watu wa kundi hili maranyingi ni wenye tabia za kuasi na ni ngumu kuwazuia au kuwatuliza. Wanandoto na maono makubwa,wanasukumwa kwa kasi na kiu zao ingawa wanaweza kuwa wakali na wasumbufu na mara 

nyingine ngumu kukaa na kuzoeana nao. Wanakisimamia sana kile wanachokiamini hata kama ulimwengu mzima usimame kinyume nao.

Mazuri yao

Wanasukumwa katika kufikia malengo yao, wako kasi kiutendaji,wanapenda raha,wana hisia nzito , wanayatazama maisha katika mtazamo chanya , wanaweza kujisimamia na kujitegemea na hawahitaji ushirika au kukubaliwa na wengine.
Mapungufu yao

Wabinafsi sana,mara nyingine wanakwepa majukumu yao,wagumu sana kusamehe,wasumbufu,wanaweza kuwa wakatitili na wenye hasira za haraka.
Maisha yao kijamii

Maranyingine ni ngumu kushirikiana nao au kuwa nao maana wanapenda kufanya mambo yao wenyewe.
Kazini

Ingawa wanaweza kuwa na malengo mengi na maono pia lakini wanaweza kuwa wasumbufu na wagumu katika kushirikiana nao kazini. Ni ngumu kufanya nao kazi maana wanataka kufanya pekeyao.
Mahusiano na mapenzi

Unaweza kufurahi nao sana kwenye mapenzi lakini uwe tayari kuvumilia hasira zao kali na za ghafla. Vumilia hali yao ya kukwepa majukumu pia,fahamu kuwa wanaweza kuwa wakali, wakatili na wasio maanisha kile wanachokisema.

Baadhi ya ukweli wa kitafiti kuhusu watu wa kundi B.

Wanatabia ya utukutu.
Pamoja na baadhi ya mazuri yao bado wanaweza wasiwe watu wazuri kwenye kuwa mume, au kuwa wapenzi wazuri kwa wasichana wao. Hii ni kutokana na urahisi 

wa tabia za kukosa uaminifu kimapenzi na urahisi wa kuumiza mioyo ya wengine.
Wanatabia ya kupenda wanyama “they love pets”
Wana kinga kubwa na imara ya mwili katika kujikinga na magonjwa.
Wanafurahia zaidi vyakula vitokanavyo na wanyama kama vile maziwa “dairy products” n.k

Damu kundi “AB”

Kundi hili ni watu wenye haiba mchanganyiko, hawa huwa na tabia tofauti kuanzia kuwa waoga na wenye aibu hadi wengine ni wapenda mitoko na wacheshi,wako 
wanafanya mambo kwa kuongozwa na mawazo na wengine hawawazi kabisa kile wanacho taka kukifanya,hii inafanya watu wa kundi hili kuwa watu wa kushangaza sana mara unapokuwa nao.

Mazuri yao

Ni rahisi sana kuwa rafiki nao.
Wanachukuliana na mazingira haraka na kwa urahisi.
Wenye kufurahisha unapokuwa nao ingawa ni watu wasiotabirika.
Wana mawazo,wana akili sana,hupenda kuweka mambo yao kwa vitendo na pia huongozwa na misimamo ya kifikra.

Mapungufu yao

Wagumu katika kufanya maamuzi.
Wanasahau sana
Ni wenye hisia za kayumba “mood swing”, mara wana furaha mara wamekasirika.
Sio waaminifu.
Ni wapinzani,wabishi na wakosaji.
Ni watu wabinafsi.

Maisha ya kijamii

Wanaweza kuwa marafiki wazuri na wenye kufurahisha.
Maongezi yao ni yenye kuhamasisha nayenye akili na kufikiria kwa hali ya juu.
Kwa kutokuwa wenye kutabirika, wengine huhofia 

kuumizwa kihisia au kukatishwa tamaa au kuumizwa moyo na watu hawa, hususani pale wanapokuwa sio waaminifu.
Kazini
Wanaweza kuwafurahisha na kuwapa burudani mnapofanya kazi nao lakini sio watu wa kuwategemea sana,wanaweza kukuangusha kirahisi.

Mahusiano ya mapenzi

Kuwa katika mahusiano na mtu wa kundi la damu la AB kunaweza kuwa kwenye kufurahisha,unaweza usiwena nyakati nyingi za upweke. Pamoja na haya fahamu kwamba watu hawa wanaweza kuwa wabishi na 

wakosoaji na maranyingine maneno yao yanaumiza. Mpenzi wa mtu au watu wa hivi lazima aelewe jinsi hisia zao zilivyo na zinavyobadilika mara kwa mara,na pale inapobidi basi uwetayari kuwapa nafasi wanayostahili ili usijiumize sana.

Baadhi ya ukweli wa kiutafiti kuhusu watu wa kundi hili.
Ni watu wazuri kwenye mambo yahusuyo fedha.
Maranyingi wanajihusisha na wanaopendendelea shughuli za kisanaa au mambo yenye sanaa ‘arts’

Ni watu wanaoaminika kuwa wabinafsi zaidi hata katika uchangiaji wa damu,watu hawa wanaweza kupewa damu na mtu mwingine yeyote ila wao hawawezi kumpa damu yeyote isipokuwa mwenzao wa AB.

Kama walivyo watu wa kundi ‘A’ na kundi ‘B’,watu wa kundi la damu ‘AB’ hupendelea vyakula vya mboga mboga “vegetables” na pia vyakula vitokanavyo na wanyama “dairy products”

Kundi la damu aina ya O.

Hawa mara nyingi wanajitahidi kuwa mahodari na mashujaa katika mambo tofauti. Mara zote kiu yao ni kuwafurahisha na kuwapendeza watu wengine ni wenye moyo wa uongozi wenye kiu ya kuwaona rafiki zao 

wakiwa wenye furaha wakati wote. Sio wagumu wa mabadiliko, wako tayari kubadilika, ni wenye mawazo mapana naya wazi, sio wagumu kifikra na ni marafiki wazuri.

Faida zao

Ni wenye ujasiri, wanashindana katika mambo mengi mfano mambo ya maendeleo, hufanya kazi sana na kwa bidii, ni waaminifu, wanaweza kujieleza, ni marafiki wazuri, wanasamehe, mitazamo yao ni chanya, huweza kuhisi au kuonamambo hata kabla hayajatokea,wanakiu ya kufahamu na kudadisi na pia niwatu wema na watoaji.

Mapungufu yao

Maranyingine wanaweza kuwa wenye fujo, wanaopenda sifa, wanavutia vitu upande wao, wanaepuka au kukwepa majukumu,unaweza kuona hawa wanaigiza mambo, wakitaka wametaka hadi wapate na nirahisi kuwaondoa kwenye kile wanachokifanya “easy to be distracted”.

Maisha ya kijamii

Ni marafiki wazuri na unaoweza kuwategemea, ni waaminifu, ni wawazi,ingawa mara nyingine wanaweza kukuudhi, pia wakati mwingine wanatamani kusikilizwa wao tu.
Kazini

Wana kiu ya mafanikio, hufanya kazi kwa bidii ingawa kukatishwa tamaa na kupoteza hamasa ya kazi kirahisi sana. Mara nyingine ili wafikie malengo ni vema wakisimamiwa kwenye kazi wanayo fanya badala ya kuachwa wafanye wenyewe..

Mahusiano ya mapenzi

Ni watu wenye mvuto wa kimahaba pia watu hawa wana hisia Kali za kimapenzi wanaweza kuonyesha mapenzi kwa wale wanaowapenda ila ni vema ukafahamu kuwa watu hawa hutarajia upendo wa jinsi ile ile wao wanavyoonyesha upendo kwako bila hivyo utakosana nao.
Ukweli wa kitafiti kuhusu watu hawa
HAWAPATI MARADHI KIRAHISI

Kwanza ifahamike kuwa watu wenye damu kundi hili wamegawanyika mara mbili ambazo ni damu kundi “O” chanya (O positive) na kundi “O” hasi (“O” negative) mgawanyo huu umetokana na mgawanyo wa kitaalamu 

ambao huitwa “rhesus factors” ambao ndio unaotumika kugawanya makundi ya damu.
Kwa ujumla kundi hili la damu liwe hasi au chanya halina proteins maalumu zilizomo ndani ya damu ambazo huitwa “antigens” ambazo ndizo mara nyingi ni rahisi 

kushika magonjwa isipokuwa lina “antibody” ambazo ndizo kinga mwili zinazopambana na maradhi ndiyo maana damu kundi “O” linaitwa “Universal Donor” damu kundi lolote linapokea.

Na kwa wakati fulani maradhi yanayowasumbua watu wenye damu kundi hili ni malaria, kichwa na mafua na wengine husumbuliwa sana na ugonjwa wa kutoka damu za pua (Rhinits) au wengine huita kambaku ambao 

husababishwa na kula nyama yenye lehemu nyingi (cholestrolel) ambazo ni nyama ya ng’ombe, kondoo, samaki aina ya dagaa, uwono na mboga ya majani inayoitwa kisamvu na wakati mwingine maziwa ya ng’ombe au kutembea kwenye jua kali sana au kutumia manukato yenye harufu kali.

NI WAPENDA NGONO

Watu wenye damu kundi hili wana hisia kali sana za mapenzi hii ni kutokana wana homoni nyingi, hali hii inawapelekea kupenda sana ngono na vile vile huwa 

wakizaa wanafanana sana na watoto wao iwe sura, tabia au mwendo iwe mwanamke au mwanaume 
Watu hawa Mara nyingi huwashwa masikio yao kwa ndani hivyo Mara nyingi wanajikuna masikio
Wanaaminika huwa na tabia za kijeshi.

Wengi wao kwa asili ni watu wa kupenda michezo.
Wanaaminika kuwa watu wema na waliotayari kusaidia mtu yeyote, hata katika uchangiaji wa damu ‘watu wa kundi ‘O’, wanaweza kumpa damu mtu mwingine yeyote.
Wanapendelea na kujisikia raha wanapokula nyama “meet lovers”.

MKRdezign

{facebook#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {twitter#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {google-plus#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {youtube#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {instagram#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL}

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget