UGONJWA WA KICHOCHO I Dr.Kimario

UGONJWA WA KICHOCHO I Dr.Kimario

UGONJWA WA KICHOCHO

Ugonjwa wa kichocho, ni ugonjwa unaosababishwa na vimelea vinavyojulikana kwa kitaalamu kama schistosoma. Ugonjwa huu huathiri zaidi ya watu milioni 207 duniani na kati ya hao asilimia 85% ni katika bara la Afrika. Baada ya ugonjwa wa malaria na maambukizi ya minyoo, kichocho ni wa tatu katika magonjwa makubwa ya kitropiki.
Kichocho ni ugonjwa ambao huathiri eneo fulani la jamii au eneo fulani la kijiografia kwa kitaalamu tunaita endemic, ambapo watu wanaathirika kutokana na shughuli zao za kila siku mfano wakulima, wavuvi, na vilevile kutokana na starehe kama kuogelea kwenye bwawa lisilo salama au ziwani.

Maambukizi ya ugonjwa huu wa kichocho hutokea pale mabuu (larvae) ya vimelea vya shistosoma yalioachiwa kutoka kwa konokono wa majini yanapopenya ngozi ya mtu aliye kwenye maji yalioathiriwa.
Ndani ya mwili wa binadamu haya mabuu (larvae) huendelea kukomaa na kuwa vimelea kamili, vimelea hivi hupenda kuishi kwenye mishipa ya damu, vimelea jike hutaga mayai, ambapo baadhi ya mayai hutolewa kwa kukojoa au kwa njia ya haja kubwa. Na mzunguko huendelea.
Kuna aina ngapi za kichocho?
Kuna aina mbili za kichocho ambazo ni:
  • Kichocho cha utumbo ama intestinal schistosomiasis na
  • Kichocho cha mfumo wa mkojo ama urinary schistosomiaisis
Kila aina ya kichocho kinaletwa na aina tofauti za vimelea hawa wa schistosoma kama ifuatavyo:
  • Kichocho cha Utumbo (Intestinal schistosomiasis) husababishwa na vimelea vya Schistosoma mansoni  na Schistosoma intercalatum
  • Kichocho cha Utumbo aina ya Asia (asian intestinal schistosomiasis) husababishwa na vimelea aina ya Schistosoma japonicum na Schistosoma mekongi
  • Kichocho cha mkojo (Urinary schistosomiasis) husababishwa na vimelea jamii ya Schistosoma hematobium
Dalili za kichocho
  • Maumivu ya tumbo
  • Kuhara damu hasa kwa kichocho cha utumbo
  • Kukojoa damu (terminal hematuria) hasa kwa kichocho cha mkojo
  • Kikohozi
  • Homa
  • Uchovu
  • Ngozi kuwasha (cercarial dermatitis) kwa jina lingine swimmers itch
Vipimo na Uchunguzi
  • Kuangalia uwepo wa mayai ya vimelea kwenye mkojo na kinyesi kwa kutumia Hadubini.
  • X-ray ya tumbo
  • Ultrasound ya tumbo
  • Kipimo cha damu (complete blood count)
  • Cystoscopy kwa kichocho cha mkojo
  • Sigmoidoscopy/proctoscopy kwa kichocho cha utumbo
Matibabu
  • Kichocho hutibiwa kwa kutumia dozi ya mara moja ya dawa iitwayo Praziquantel
Madhara ya Kichocho
  • Kansa ya kibofu cha mkojo (cancer of urinary bladder)
  • Figo kushindwa kufanya kazi
  • Cor pulmonale
  • Gastrointestinal bleeding - Kuvuja damu ndani ya mwili hasa katika mfumo mzima wa chakula
  • Portal hypertension
  • Seizures - Kifafa au degedege
  • Reflex nephropathy
Jinsi ya kuzuia kichocho
  • Kuondoa na kuangamiza konokono waliopo kwenye maji au ambao hupenda kuishi kwenye maji ambao ni muhimu katika mzunguko wa kuuwaji wa vimelea vinavyoleta kichocho kwa kutumia Acrolein, copper sulfate na niclosamide.
  • Kwa sasa kuna utafiti unaendelea kwa ajili ya kutafuta chanjo ya ugonjwa huu wa kichocho.
Labels:

Post a Comment

[blogger][facebook][disqus]

MKRdezign

{facebook#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {twitter#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {google-plus#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {youtube#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {instagram#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL}

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget