December 2019

Baada ya kujifungua, baadhi ya akina mama hutoa maziwa kidogo sana kwa ajili ya watoto wao na wengine hukosa kabisa maziwa.
Hali hii huleta changamoto kubwa kwani mtoto huanza kulia sana na wakati mwingine kuishiwa maji mwilini na kuchemka.
Kitaalamu baada ya kujifungua homoni nyingi za uzazi zinapungua kisha homoni zingine kwa ajili ya uzalishaji wa maziwa kitaalamu kama prolactin hutengenezwa, sasa kuchelewa kwa kwa hatua hii kunaweza kuleta shida hii.


mambo gani unaweza kufanya kutibu tatizo hili?
usiishiwe na maji mwilini: hakikisha unakunywa maji ya kutosha angalau glass nane kwa siku ili kuongeza kiasi cha maji mwilini mwako.
kumbuka maziwa yako kwenye mfumo wa kimiminika hivyo maji mengi yanahitajika kuyatoa.
kula mlo kamili; ungeza ulaji wako wa zamani kwa zaidi kidogo, vyakula vya protini kama mayai, nyama,maziwa nay ng'ombe samaki na mboga za majani husaidia sana sana kuzalisha maziwa ya kutosha ambayo yanaweza kukidhi mahitaji ya mtoto.
tumia virutubisho; taasisi  nyingi za kiafya zinashauri matumizi ya madini ya clacium, vitamin D, Iron, na folic acid kama kiungo muhimu sana katika kumuandaa mama kuzalisha maziwa mengi na yenye virutubisho vya kutosha ndani yake.
nyonyesha mara kwa mara; hata kama maziwa ni kidogo sana jitahidi kumnyonyesha mtoto mara nyingi sana iwezekanavyo yaani mara 10 mpaka 12 ndani ya saa 24 au kila anapohitahi na hii itasaidia sana kutengeneza homoni ya oxytocin ambayo husaidia sana kutengeneza maziwa.
nyonyesha ziwa moja moja; ukimpa mtoto ziwa moja mpaka maziwa yakaaisha kabisa, taarifa hutumwa kwenye ubongo kwamba maziwa yameisha kabisa hivyo ziwa lingine litajazwa maziwa haraka wakati mtoto anamalizia kunyonya ziwa lingine.
matumizi ya dawa; wakati mwingine baadhi ya dawa hutumika hasa pale kiwango cha homoni inayohusika na maziwa inapoenekana iko chini sana na haiwezi kuongeza kiwango cha maziwa.
dawa ya dompiredone huweza kutumika kwa dozi ya 10mg kutwa mara nne na kuongeza mpaka kiwango cha mwisho cha 20mg kutwa mara nne.
Mama anaweza kupunguza dozi na kuacha kabisa kama maziwa yakipatikana, ila ikitokea maziwa yanapungua tena basi ataanza dozi na kuendelea nayo mpaka atakapomuanzishia mtoto vyakula vingine, mara nyingi baada ya miezi sita.
mwisho; wakati mwingine mama anaweza asipate nafuu pamoja nakutumia dawa zote, huenda sababu ya vyanzo vingine ambavyo vinakua nje ya matibabu kama historia ya upasuaji wa matiti na kadhalika hivyo anaweza kutumia maziwa mbadala ya lactogen au maziwa ya ng'ombe .

Kwa miaka mingi imekua ikifahamika kwamba kuosha sehemu za siri baada ya tendo la ndoa kuna zuia magonjwa ya zinaa kama kaswende, pangusa na mengine ambayo huambukizwa kwa tendo la ndoa, hii imekua ni kweli kwasababu magonjwa ya aina hiyo huhitaji muda wa kutosha kuweza kuanzisha makoloni yao sehemu za siri ili kuleta ugonjwa.
hivyo maji maji yenye ugonjwa huo yakishaoshwa yanasimamisha mfumo mzima wa kuanzisha ugonjwa husika.



Lakini hii imeonekana ni tofauti linapokuja swala la virusi vya  ukimwi kwani kuosha sehemu za siri hasa kwa wanawake na wanaume ambao hawajatahiriwa kumeonekana kuongeza maambukizi badala ya kupunguza.
Utafiti huu ulifanyika nchini Uganda ulichukua wanaume ambao hawajatahiriwa ambao wanatabia hiyo kisha kuchukua wanaume ambao hawana tabia hiyo na kuwafuatilia kwa muda Fulani( cohort studies) na majibu yakionyesha kuongezeka kwa maambukizi kwa 2.3% kwa wale wenye tabia ya kuosha uume wao muda mfupi tu baada ya tendo la ndoa.
Lakini utafiti mwingine ulifanyika nchini kenya kwa muda wa miaka kumi kwa wanawake 1270 na majibu yalionyesha kuongezeka kwa maambukizi ya ukimwi kwa asilimia 2.6% kwa wale walio osha sehemu zao za siri pale pale ukilinganisha na wale waliochelewa na kuosha baada ya dakika kumi mpaka 20.

je chanzo cha maambukizi haya ni nini?
Hakuna majibu ya uhakika wa swali hili lakini wataalamu wamekuja na ababu ambazo huenda ndio zinachangia kutokea kwa jambo hili kama ifuatavyo.
kuongeza ukali wa virusi; sehemu za siri za mwanamke zina maji maji ambayo yana tindikali ambayo kazi yake ni kuua wadudu ambao wanaingia ndani ya uke, sasa ukimwaga maji pale ile tidikali inaishiwa nguvu na kuwapa virusi wale nguvu.
kuongeza michubuko; baadhi ya watu huosha na sabuni au dawa mbalimbali,yale maumivu kidogo unayosikai baada ya kumwaga maji au kupaka sabuni ni kuongezeka kwa michubuko ambayo inatoa nafasi zaidi kwa virusi vya ukimwi kufanya mashambulizi.
kuvipa virusi uwezo wa kuishi na kusafiri; kwa kawaida virusi huishiwa nguvu au kufa pale maji maji yanayovizunguka yanapokauka, kuosha na maji na kuongeza maji maji na kuvihamisha sehemu zingine za sehemu za siri ambazo huenda zina michubuko Zaidi.
mwisho;Kwa lugha nyingine sio vizuri kuosha sehemu za siri muda mfupi tu baada ya tendo la ndoa, jipe muda wa kutosha kitandani na mtu wako kama dakika 10 au 20 ukiwa umepumzika au unafanya mambo mengine kisha unaweza kwenda kunawa.

MKRdezign

{facebook#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {twitter#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {google-plus#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {youtube#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {instagram#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL}

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget