September 2020







Eczema (atopic dermatitis) ni ugonjwa wa ngozi ,unaofanya ngozi kuwasha sana kuwa kavu na kupata vijipele vidogo vidogo vyenye rangi nyekundu,huu ugonjwa ushambulia watoto na wakubwa sehemu za viungo vya mwili (joints) mkononi

Shingoni na miguuni na inaweza tokezea sehemu ya usoni ,juu ya jicho ,makwapani,mgongoni ,tumboni ,mbele ya kichwa (forehead),mapajani,mdomoni na mashavuni. Watoto walio chini ya miaka 5 huwa adhiri kwa asilimia 15% unaweza chukua mda kupona kulingana na ngozi na kiasi cha mtoto alivyoadhirika.

Chanzo cha ugonjwa wa eczema

Eczema inasababishwa na mwili kushindwa kutengeneza au kuzalisha ceramider ,ceramider ni fatty cell inayotumika kwenye uzalishwaji wa ngozi,ceramider inaposhindwa kuzalishwa ngozi ya mtoto inapoteza kiwango cha maji na kuifanya kuwa kavu na ndipo inapo msababishia kuanza kujikuna ,ngozi kuwa kavu na kubadilika rangi kuwa nyekundu.

Eczema ni ugonjwa wa kuridhi -toka kwa mama / baba aliekuwa na ugonjwa ni rahisi mtoto akaridhi.

Mzingo(Allergy au asthma)na pumu huleta eczema

Mtoto anaweza pata allergy ya vyakula tofauti kama maziwa,mayai,ngano,soya samaki,nyaman.k na baadae kumpelekea kupata eczema.

Nini kinachochea kutokupona eczema haraka kwa mtoto

Mtoto mwenye tatizo la eczema anatakiwa aepushwe

Ngozi kuwa kavu (dry skin)-epuka ngozi ya mtoto kuwa kavu itasababisha kuwa na low humidity na kujikuna sana .

Joto kali-joto linapokuwa kali inamsababisha mtoto kujikuna zaidi ,usimveshe mtoto nguo nyingi kipindi cha joto itamfanya ajikune sana .

Food allergy-kuna baadhi ya vyakula vyenye kuleta allergy inatakiwa asipewe kama maziwa,mtindi,mayai,cheese ,nuts(karanga,korosho nk)mikate,pweza,kamba

Acid fruits-matunda ya acid asitumie ndimu ,machungwa,nyanya,strawbell

Acha kutumia vitu vya harufu kali kama sabuni ,perfumes ,majani,na mafuta kwenye mwili wake na nguo zake

Kuogeshwa kwa mda mrefu-epuka kumwogesha kwa mda mrefu au kukaa ndani ya maji isizidi dakika 10 maji yana sababisha ngozi kuwa kavu zaidi,atumie maji vugu vugu wakati wa kumwogesha tumia sabuni ya (sensitive skin) isiyo na harufu na usitumie shampoo

Nguo za kumbana-usimveshe nguo za kumbana au zenye material ya synthetic fabric, wool, ,mveshe nguo za kupwaya ziwe material ya cotton inamfanya ajisikie vizuri bila miwasho.

Nguo mpya-nguo mpya inamfanya ajikune zaidi ,kabla ujamvesha fua kwanza.

Sabuni ya kufulia nguo -nayo inaweza msabishia kuwashwa zaidi ,fatilia kila ufuapo kama ukimvesha izo nguo na kuwashwa sana ujue iyo sabuni haimfai

Kucha kuwa ndefu-zitamkwarua na kujikuna sana kuharibu ngozi zaidi ,hakikisha kucha zake ni fupi kila mara.

Kutompa daily products zozote zitokanaza na ng’ombe au kuku (maziwa,mtindi,mayai,cheesen.k)

Vizuri umpeleke hospital Kupima allergy ili ujue , kama anayo ni rahisi kumwachisha kumpa vyakula vinavyompa allergy mapema kabla hajawa eczema.

Tiba

Eczema kutibika kwa haraka ni ngumu ,kuna dawa za kupaka na ikapunguza muwasho, fatilia masharti hayo nilioandika hapo juu na kula matunda na mboga mboga kwa wingi

Yanayoweza tibu au punguza eczema kwa kiasi kama parachichi ,ndizi mbivu, papai,apple,juice ya carrots ,tango,aloe vera,spinanch ,viazi vitamu,viazi ulaya,smoothie ya tango,parsley.Broccoli na tangawizi unaweza saga pamoja na kumpa mtoto ila kwa wale walio juu ya miezi 6 na kuendelea.

Samaki wa maji baridi kama salmon wanafaa zaidi wana omega 3 ya kutosha.Mwepushe mtoto kula fast food zinachochea ugonjwa kuongezeka

Tiba ya kutibu haya Maradhi ipo kwamtu mwenye kutaka unaweza kunitafuta kwa wakati wako.

Ukiwa na Shida yoyote ile

Usipo pona kwa Dawa za Hospitali nitafute mimi nipate kukutibia upate kupona ukinihitaji matibabu yangu

Unaweza kunitafuta kwa Mawasiliano Herbalist Dr. MziziMkavu What's App +447459370172


 







 



Na. Catherine Sungura,WAMJW-Tabora

Imeelezwa kuwa kuboreshwa kwa miundombinu imesaidia kwa kiasi kikubwa huduma ya damu salama kwenye Kanda ya Magharibi ambayo inahudumia mikoa ya Tabora,Katavi,Singida na Kigoma.

Kaimu Meneja wa kanda hiyo Bi. Zaitun Abdalah ameyasema hayo wakati wa kampeni ya kukusanya damu kwenye shule ya sekondari Mabama iliyoko Manispaa ya Tabora.

“Kwa kiasi kikubwa uboreshwaji wa barabara umesaidia sana kurahisisha upatikanaji wa mahitaji wa damu salama kwenye mikoa hii tunayoihudumia ambayo inayo eneo kubwa kijiografia hivyo inapohitajika damu kwenye vituo vyetu vya kutolea huduma tunawapatia kwa wakati”Alisema.

Kwa upande wa wiki hii ya kampeni ya kukusanya damu iliyoanza tarehe 21 mwezi huu na kumalizika tarehe 25 ,Kaimu Meneja huyo amesema Kanda yake imeweza kukusanya chupa 186 kwa siku mbili ikiwa imekaribia lengo lililoweka la kukusanya chupa 100 kwa siku na chupa 500 zinazotarajiwa kukusanywa kwa wiki.

Aliongeza kuwa kwa mkoa wa tabora timu yake imejipanga katika ukusanyaji wa damu katika wilaya ya Igunga na timu nyingine katika manispaa pamoja na halmashauri ya wilaya ya Uyui na wamelenga kuwafikia wanafunzi wa sekondari kwani upatikanaji wa kundi hilo ni rahisi katika kipindi hiki.

“kama kanda hatujachoka kuhamasisha wananchi licha ya changamoto ya uelewa kwa jamii kuhusu uchangiaji damu,hivyo tumejipanga kuendelea kutoa elimu kwenye makundi yote ili tuweze kuwa na damu za kutosha kwenye hospitali zetu”.

Hata hivyo alisema kama Kauli mbiu ya kampeni hii  inavyosema “changia damu,ili kuokoa maisha ya akina mama wanaoleta uhai duniani “hivyo jamii inapaswa kuelewa uchangiaji wa damu mara kwa mara ni muhimu ili kuokoa vifo vya akina mama wajawazito  wanapoteza uhai wakati wanapotimiza haki yao ya kuleta watoto duniani. 

Naye Afisa Mhamasishaji wa kanda hiyo Constantine Chiba alisema wamejiwekea utaratibu kutoa elimu ya kuchangia damu kwa kutembelea vijiji mbalimbali kwenye mkoa huu,nyumba za ibada pamoja na makundio mengine katika jamii ili kuweza kuwa na akiba ya damu na pindi inapohitajika waweze kuokoa maisha ikiwemo ya akina mama wanaojifungua.

Chiba alisema yapo makundi matano ya wahitaji wa damu yakiwemo akina mama akina mama wajawazito na watoto wachanga,wahanga wa ajali,wanaohitaji tiba ya upasuaji,wenye matatizo ya kuishiwa damu (sikoseli) na kundi la mwisho ni watu wote ambao wanaweza kuugua na kuhitajika kuongezewa damu“kumbe sisi sote ni wahitaji wa damu kwani hatuyawezi kuyakwepa makundi haya yote kama binadamu kwani ugonjwa au ajali haiwezi kukwepa jinsia au umri wa mtu”.









Na. WAMJW-Singida


WIZARA ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imewakumbusha wauguzi wote nchini kuhakikisha wanajiendeleza kielimu, ili baadae wawe na maarifa zaidi ambayo yatawaongezea ubunifu na utendaji wao wa kazi. 

Wito huo umetolewa leo na Mkurugenzi wa huduma za Uuguzi na Ukunga kutoka wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ziada Sellah, kwenye mkutano baina yake na wauguzi na wakunga wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Singida.

Mkurugenzi huyo licha ya kusisitiza umuhimu wa kujiendeleza kielimu, pia amewapongeza watumishi wa kada ya uuguzi mkoani Singida, kwa kutekeleza vema majukumu yao, licha ya kukabiliana na changamoto mbalimbali wakiwa kazini.

"Niwapongeze wauguzi wote kwa jitihada zenu mnazofanya kila siku za kuwahudumia wananchi,mmekua  muda mwingi mko na wagonjwa na hamchoki kutoa huduma kwa rika zote"Alisema Bi. Sellah

Alisema Wizara ya Afya inatoa udhamini kwa masomo ya ngazi za juu kwa watumishi wa sekta ya afya kila mwaka,hivyo wanapaswa kuomba nafasi hizo bila kusita.

Naye Muuguzi mkuu wa mkoa wa SINGIDA Hyasinta Alute, amesema kuwa hospitali na vituo vingi vya afya mkoani humo havina magari ya kubebea wagonjwa, hali inayohatarisha maisha ya wajawazito wanaopata rufaa, huku muuguzi mfawidhi wa hospitali ya rufaa ya mkoa Theresia Ntui, akiwaasa wauguzi kufanya kazi kwa weledi ili kuokoa maisha ya wagonjwa wanaofika Hospitalini hapo kupata huduma.



Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Abel Makubi


Na.WAMJW-Dodoma

Mganga Mkuu wa Serikali Prof.Abel Makubi amewataka Waganga Wakuu wa Mikoa, Wilaya, Wakurugenzi wa taasisi, vyuo vya afya, na waganga wafawidhi kuhakikisha wanawafuatilia kwa karibu wanataaluma wa afya walio katika mafunzo kwa vitendo , yaani watarajali (interns) ili waweze kupata umahiri(competences), utalaamu(skills) na maadili yanayotegemewa. 

Prof. Makubi ameyabainisha hayo wakati akiongea na wasajili wa Mabaraza ya kitaaluma yaliyopo chini ya wizara afya katika ukumbi wa wizara jiji hapa.

Prof. Makubi alisema Serikali imeenza kupata changamoto za baadhi ya Hospitali kushindwa kuwapa mafunzo stahili  wataraji hao na kujikuta wanamaliza mafunzo yao bila umahiri unaotegemewa katika kutoa huduma kwa wananachi.

"Serikali imeanza kuchunguza hizo hospitali na kama hazitasimamia vyema hawa wanataaluma walio mafunzoni, tutazifutia kibali cha kuwapokea"Alisisitiza 

Aidha, Prof. Makubi aliwataka wanafunzi walio kwenye mafunzo kwa vitendo kujituma katika mafunzo yao, kuonyesha nia ya kujifunza na kuweka bidii katika mafunzo yao ya vitendo mahali walipo. 

"Hawa wanataaluma wanapaswa kuonyesha tabia njema wakati wa mafunzo, kuwa watiifu, kulinda viapo vyao kuzingatia maadili ya taaluma zao na kujiheshimu katika lugha zao na hata mavazi wanayovaa mbele ya wateja wao ambao wengi ni wagonjwa na ndugu zao"Aliongeza. 

Hata hivyo Prof. Makubi ameyaagiza mabaraza hayo kuhakikisha utaratibu wa watarajali 'interns' wote kufanya mitihani baada ya mafuzo, uharakishwe ndani ya   mwaka huu ili serikali iweze kupima umahiri wa wanataaluma wote wanaomaliza mafunzo kwa vitendo.

Prof. Makubi aliipongeza Baraza la  Famasi  kwa kuratibu mitihani kwa wafamasia wataraji  na kulitaka  Baraza la Madaktari nalo likamilishe utaratibu wa mitihani kwa madaktari watarajali wote ili kulinda hadhi ya taaluma ya tiba na viwango vya kutoa huduma kwa wananchi.





Mganga Mkuu wa Serikali wa Serikali Prof. Abel Makubi

Na. WAMJW-Dodoma

Wanataaluma wote wa sekta ya afya nchini wametakiwa wawe wamejisajili, na kuhuisha leseni kwenye mabaraza yao ya kitaalam ndani ya miezi sita kuanzia sasa. Aidha kwa wale ambao wamejiendeleza zaidi kitalaamu wanatakiwa kuwasilisha(update) vyeti vyao vya viwango katika mabaraza ili kutambulika kisheria na kitaaluma. 

Rai hiyo imetolewa leo na Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Abel Makubi wakati akiongea na wasajili wa mabaraza mbalimbali ya kitaalam ya Wizara ya Afya pamoja na wasajili wa bodi zilizo chini ya wizara hiyo.

“Kila mwanataaluma aliyemaliza mafunzo yake ni vizuri awe amesajiliwa katika mabaraza yao, agizo hili ni kwa wanataaluma wote katika sekta ya afya ili muweze kutambulika, na uzuri hivi sasa kuna tovuti hivyo mnaweza kupata kujisali , kulipia na baadae kutumiwa  vyeti vyenu bila kuchelewa.  Kwa mantiki hiyo nawapa miezi sita wawe wamesajiliwa”. Alisisitiza

Pia wanatataaluma wanaojiendelea kwa ngazi mbalimbali ya taalauma ya afya kama uzamili na uzamivu 'PhD’ wanatakiwa kusajili hivi viwango katika mabaraza yao ili watambulike. 

Prof. Makubi amesema utaratibu huo umewekwa na Serikali kupitia mabaraza hayo hivyo kila mwana taaluma anatakiwa kujisajili au kuhuisha leseni ambazo zimeisha muda ili waendelee kutambulika na kufanya kazi zao.

Aidha,Prof. Makubi ameongeza kuwa wizara kupitia mabaraza hayo imeweka miundombinu ya mafunzo endelevu ya kitaaluma kwa kila taaluma kwa kufanya mitihani kwa ngazi zote."Lakini mtu aliyefanya mtihani nje ya utaratibu huu basi anatakiwa kuleta  ili kufanya usajili ili kupata alama na uwekwe kwenye kiwango stahili na ndio utaonekana bado upo kwenye kiwango cha uelewa kwenye taaluma yako na kuwatumikia wananchi”.

Kwa upande wa baadhi ya watu wa sekta ya afya wanaojipa hadhi ya kiwango fulani cha taaluma bila ya kujisajili kwenye mabaraza ya kitaaluma, Prof. Makubi ametoa miezi mitatu kwa wale wanataaluma wenye vyeti vyao wajisajilii ili kutambulika wapo katika kiwango fulani cha taaluma. 

“Kuna baadhi ya wataaluma wanaojipa hadhi ya kiwango fulani cha kitaaluma wakati hawajasajili vyeti vyao  kwenye mabaraza, nitoe mfano kuna wanataaluma wanaojiita mabingwa wa kitu fulani (specialist, consultant …) na wanajitangaza kwa wananchi wakati hatuna ushahidi na kumbukumbu. Kwahiyo tumekubaliana na mabaraza suala hilo sasa lifikie mwisho na wote waliojiendeleza zaidi waje wajisajili haraka kwa kuwasilisha vyeti vyao.” Alisisitiza Prof. Makubi.

Hata hivyo Mganga Mkuu wa Serikali aliwaagiza waganga wakuu wa mikoa, wilaya, wakurugenzi wa Hsopitali, taasisi za afya, vyuo vya afya na waganga wafawidhi wote kuzingatia kusimamia utekelezaji wa maagizo haya kwenye sekta zote za afya ili kulinda viwango na hadhi ya taaluma husika. “Taaluma zote za afya lazima ziendelee kuheshimika na kusimamiwa vizuri ili kulinda afya za wananchi kwa viwango vya juu na bila kuruhusu wanataaluma bubu”, Alisema Prof Makubi.

Pia kwa Waganga wa tiba asili wametakiwa kufuata utaratibu wa kujisajili pamoja na wasaidizi wao na kufuata miongozo ya utoaji wa tiba asili na tiba mbadala kwani serikali ipo tayari kuwapa ushirikiano kwa kuwasaidia malengo yao ya utoaji wa tiba asili yanafanikiwa.

-MWISHO-



Mkurugenzi wa Huduma za Kinga Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto 
Dkt. Leonard Subi

Na Gerard Chami - WAMJW, Arusha. 

Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imefanikiwa kutokomeza mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu (Cholera) hapa nchini.


Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Huduma za Kinga Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Leonard Subi wakati akizindua kikao kazi cha kufanya tathmini, maboresho na kuandaa mpango kazi wa miaka mitano katika kukabiliana na ugonjwa huo hapa nchini. 


“Tangu mwezi Julai mwaka 2019 hatuna kesi yoyote iliyotolewa taarifa ya kuwepo kwa mgonjwa wa Cholera hapa nchini. Kwa miaka kadhaa tumekua na takribani asilimia 11 ya vifo vitokanavyo na ugonjwa huu, lakini kutokana na kazi nzuri iliyofanyika katika maeneo tofauti ikiwemo kuimarishwa kwa miundombinu ya kutolea huduma za afya, upatikanaji wa dawa, vifaa, vifaa tiba na vitendanishi, kaya karibu zote nchini kuwa na vyoo safi na bora, kuimarishwa kwa usafi wa mazingira na upatikanaji wa maji safi na salama nchini kipindupindu kilipungua mpaka asilimia 1.7 na kwa kipindi cha mwaka jana hadi sasa hatuna mgonjwa aliyetolewa taarifa kabisa kuwa na maambukizi hayo.” Amesema Dkt.Subi 


Amesema, kazi iliyopo hivi sasa na inayopewa kipaumbele na Serikali kupitia Wizara ya Afya ni kuchambua kwa umakini mkubwa mpango kazi wa miaka mitano wa udhibiti wa ugonjwa huu, kufanya ufuatiliaji, tathmini na uperembaji wa afua mbalimbali za afya hapa nchini na kuja na mpango kazi wa utekelezaji kimkakati katika kudumisha hali hii hapa nchini kwani hivi sasa nchi imeingia katika uchumi wa kati hivyo ni vema kudumisha hali ya afya ya wananchi ambao ndiyo nguvu kazi ya Taifa katika kuleta maendeleo, kukuza kipato na kuboresha hali ya maisha ya mwananchi mmoja mmoja. 


Aidha Dkt.Subi amesisitiza kuendeleza utamaduni wa kunawa mikono muda wote kwa maji safi yanayotiririka na sabuni kwani unasaidia kukabiliana na maradhi mengine zaidi ya Corona ikiwa ni pamoja na kudumishwa kwa utoaji elimu ya afya kwa umma ili twende pamoja kama taifa linaloendelea kwa kasi. 


Akiongezea Dkt.Subi amesema ni vema kwa pamoja tukaendelea kuongeza nguvu na ushirikiano katika kulinda vyanzo na mikondo ya maji safi na salama kwani maji ni uhai na uhai ni afya hivyo itatusaidia kama Taifa kupambana na maradhi mbalimbali mijini na vijijini. 


Vilevile Dkt.Subi amesema suala la chanjo ya kuzuia kipindupindu kwasasa sio kipaumbele na badala yake nguvu kubwa inazidi kuwekwa katika kuimarisha miundombinu stahiki ya huduma za afya, usafi zaidi wa mazingira na upatikanaji zaidi wa maji safi kwa wananchi katika maeneo yote. 


Nae Mwenyekiti wa Kikao kazi hicho ambaye pia ni Mkurugenzi Msaidizi wa eneo la Ufuatiliaji na Udhibiti wa Magonjwa Dkt.Janeth Mghamba akitoa neno la shukrani kwa mgeni rasmi ameahidi kwa niaba ya timu za wataalamu wa afya kuendelea kuwashirikisha viongozi wa Serikali za Mitaa katika jamii wanazotoka (kata, mitaa na vijiji), kusukuma uimarishaji wa maabara katika ngazi zote; mkoa, wilaya, zahanati na halmashauri ikiwa ni pamoja na kuendelea kuwajengea uwezo wataalamu. 


Pamoja nae, Dkt.Faraja Msemwa kwa niaba ya Shirika la Afya Duniani (WHO) hapa nchini ameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa umoja na mshikamano uliopo kwa kuwaweka wadau wa maendeleo karibu katika kukabiliana na majanga ya maradhi mbalimbali hapa nchini na yale yanayoikumba dunia kwa ujumla wake kwani afya ni msingi wa maendeleo ya Taifa lolote. 


Mwisho Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ndg.Gerard Chami, amewataka wanahabari kuendelea kutumia vyombo vyao ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za Serikali kupitia Wizara ya Afya kuelimisha umma juu ya utunzaji wa mazingira, matumizi sahihi na utunzaji wa vyoo bora, uhifadhi wa vyanzo vya maji na kudumisha utamaduni wa kunawa mikono kwa maji safi na salama yanayotiririka na sabuni. 

Mwisho




KATIBU MKUU Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto - Idara Kuu ya Afya Prof. Mabula Mchembe akisema jambo  kwa wadau (hawapo pichani) wakati wa ufunguzi wa Siku ya Tiba ya Asili kwa Mwafrika

Dkt. Grace Magembe Mkurugenzi wa Huduma za Tiba kutoka Wizara ya Afya

Mzee Issa Mdoe Mwakilishi wa Wagaga wa Tiba asili kutoka Mkoa wa Dodoma






Na WAMJW- DOM 

KATIBU MKUU Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto - Idara Kuu ya Afya Prof. Mabula Mchembe amewaagiza Baraza la Tiba Asili na Tiba mbadala na Mamlaka zote katika Mikoa na Halmashauri nchini kusimamia usajili wa dawa za asili kwa kutoa elimu ya kutosha kwa waganga na watengeneza dawa wa tiba asili. 

Prof. Mchembe ameyasema hayo leo wakati akifungua maadhimisho ya siku ya tiba asili ya Mwafrika yaliyofanyika katika viwanja vya Mwl. Nyerere Jijini Dodoma, yenye kauli mbiu ya "Miongo miwili ya Tiba Asili Afrika 2001 mpaka 2020 Nchi zina mafanikio gani".

"Kwa maana hiyo basi nawaagiza Baraza la Tiba Asili na tiba mbadala na Mamlaka zote katika Mikoa na Halmashauri nchini kusimamia usajili wa dawa za asili kwa kutoa elimu ya kutosha kwa waganga na watengeneza dawa wa tiba asili" alisema Prof. Mabula Mchembe. 

Aliendelea kusisitiza kuwa, ni vyema Baraza la tiba asili na Mamlaka zote nchini, kushirikiana na taasisi zote zinazohusiana na tiba asili hususan Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, kutokana na kuwepo kwa kitengo kinachohusiana na mimea. 

Prof. Mchembe amesema kuwa, katika kuadhimisha miaka 18 ya siku ya tiba asili ya Mwafrika, Serikali kupitia Wizara ya Afya imefanya mambo mengi ikiwemo, kuitambua huduma ya tiba asili katika Sera ya Afya kuanzia, kutungwa kwa Sheria ya tiba asili na tiba mbadala Namba 23 ya mwaka, kutengenezwa kwa kanuni na miongozo mbalimbali ya Tiba Asili na Tiba Mbadala mwaka, kuanza kutoa mafunzo kwa Waratibu na watoa huduma wa tiba asili nchini.

Aidha Prof. Mchembe, ameliagiza Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala na Mamlaka zote katika Mikoa na Halmashauri nchini kusimamia usajili wa dawa za asili kwa kutoa elimu ya kutosha kwa waganga na watengeneza dawa wa tiba asili.

Mbali na hayo Prof. Mchembe ametoa wito kwa Wataalamu wa tiba asili na tiba mbadala nchini kutumia fursa kwa kuanzisha viwanda vidogo na vya kati vya kuchakata dawa za asili kwa lengo la kuongeza ubora na hivyo thamani yake. 

"Nitoe wito kwa Waganga na wadau wa Tiba Asili kutumia fursa iliyopo ya Tanzania ya Viwanda kwa kuanzisha viwanda vidogo na vya kati vya kuchakata dawa za asili kwa lengo la kuongeza ubora na hivyo thamani yake" alisema Prof. Mchembe 

Kwa upande wake Mkurugenzi wa tiba Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Grace Magembe amesema kuwa, kupitia maadhimisho ya tiba asili kama nchi tumepata mafanikio mengi sana ikiwemo kuongezeka idadi kubwa ya wananchi wanaotumia dawa za asili hususan katika kipindi cha mlipuko wa virusi vya Corona. 

"Kupitia maadhimisho ya tiba asili, tangu tumeanza kama nchi, Luna mafanikio mengi sana yameweza kupatikana, lakini kubwa naloweza kulisemea, ni kuongezeka kwa idadi ya wananchi wanaotumia dawa zetu za asili pamoja na tiba mbadala, na mfano mzuri ni katika kipindi cha mlipuko wa ugonjwa wa Corona, kama nchi tunaweza kusimama kifua mbele na kusema tiba zetu za asili zimetutoa kwa kiwango kikubwa, " alisema. 

Aliendelea kusema kuwa, pamoja na kuendelea na utafiti wa dawa mbali mbali za asili ambazo zilitumika katika kipindi cha mlipuko wa ugonjwa wa Corona, takribani zaidi ya watu 100,018 walitumia dawa za asili, ikiwemo njia ya kujifukiza (nyungu), na kuonesha mafanikio kwa kiasi kikubwa. 

Nae Kaimu Msajili Baraza la tiba asili na tiba mbadala Wizara ya Afya Ndg. Patrick Seme amesema kuwa, hadi sasa Baraza la tiba asili na tiba mbadala limeshasajili dawa 30, huku akiweka wazi kuwa kiasi hiki cha dawa zilizosajiliwa ni kidogo ukilinganisha na uhalisia, huku akiweka wazi kuwa Baraza linaendelea kuhakikisha linasajili dawa nyingi zaidi kwa kufuata kanuni na taratibu. 

"Kama mnavyofahamu kuwa mwaka 2017 tulianza kusajili dawa za asili kupitia Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala na kuwa hadi sasa dawa 30 zimesajiliwa. Kiasi hiki cha dawa zilizosajiliwa nichache sana ukilinganisha na uhalisia." Alisema. 

Akiwawawakilisha Waganga wa tiba asili Mkoa wa Dodoma Mzee Issa Mdoe amesema kuwa, Baraza la tiba asili na tiba mbadala kwa kushirikiana na Waganga wa tiba asili limekuwa na mafanikio mengi yakiwemo kutoa elimu mara kwa mara kwa Waganga kujua dhana ya tiba asili ikiwemo kujiepusha na mauaji ya vikongwe na mauaji ya albono na mauaji ya watoto wadogo. 

Mbali na hayo Mzee Issa Mdoe ameweka wazi kuwa, baadhi ya changamoto zinazowakumba, zikiwemo gharama za usajili wa dawa kuwa juu, hivyo kuwafanya Waganga wengi kushindwa kisajili dawa zao, elimu ndogo ya malipo ya njia ya elektroniki inayopelekea baadhi ya Waganga katapeliwa na watu wasio waaminifu.

Mwisho.



MKRdezign

{facebook#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {twitter#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {google-plus#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {youtube#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {instagram#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL}

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget